Uniimbie
Uniimbie
Si wimbo
Si shairi
Si utenzi
Uniimbie
Hisia zako na zangu
Hisia za wanaAdamu
Hisia za wavuja
jasho na damu
Uniimbie
Ya maisha bora
Yenye ustawi na Utu
Yenye mwanga bila luku
Langu Dua
Likiwaka jua
Ukiiandama mwezi
Giza litakimbia
Mende zitaparaganyika