The Banana Plant

Mgomba umelala chini: hauna faida tena, Baada ya kukatwa na wafanya kazi Wa bustani kwa kusita. Watoto, kwa wasiwasi wanasubiri wakati wao Bustanini hakuna kitu Isipokuwa upepo fulani wenye huzuni, Unaotikisa majani na kutoa sauti ya kilio.  Hivyo ndivyo ufalme wa mitara ulivyo. Mti wa mji umelala chini: hauna faida tena, Baada ya kukatwa na […]

Evening Tea

Wakati tunywapo chai hapa upenuni Na kuwatazama watoto wetu Wakicheza bembea kwa furaha Tujue kamba ya bembea yetu Imeshalika na imeanza kuoza Na bado kidogo tutaporomoka. Kulikuwa na wakati ulinisukuma juu Nikaenda zaidi ya nusu duara; Kulikuwa na wakati nilikudaka Ulipokaribia kuanguka, Na kulikuwa na wakati tulibebana kwa zamu Mmoja wima akisukuma mwingine amekaa. Wakati […]

Floods

Nitaandika wimbo juu ya mbawa za nzi Utoe muziki arukapo wausikie walio wengi Ushairi wa jalalani utaimbwa Juu ya vidonda vya wakulima Na usaha ulio jasho lao. Nitaandika juu ya mbawa za wadudu Wote warukao Juu ya mistari ya pundamilia Na masikio makubwa ya tembo. Juu ya kuta vyooni, maofisini, madarasani, Juu ya paa za […]

I Crossed

Nimevuka mabara kuja Afrika Lakini siku katu haikufika             ya milima kuwa vilima             ya mito kuwa vijito             vya kuweza kudakiika. Sijakufikia mpenzi kama kwamba u nyota ya mbali kama kwamba umemea baina yetu             ukuta wa usingizi. Nikikushika, mikono huwa haishiki ila maiti ilokufa bila haki             kama kukumbatia damu yangu jiweni             […]

The Winds of Time

Juu ya mlima mdogo Siku moja nilisimama. Nikatazama chini ziwani, siku Ya dhoruba. Halafu niliona mawimbi Yakipanda na kushuka. Yakivimba, Yakiviringika, yakigongana na kutoa povu Kama fahari wehu katika bonde lisomajani. Yalivyotengenezwa! Yalivyofifia na kuanza tena! Kamwe sikuona. Lakini niliyaona yakishuka kwa nguvu Na kupanda haraka, yakisukumwa Na upepo wa Magharibi na Mashariki. Hivyo ndivyo […]

I Am I

Waniita mkomunisti Waniita mkapitalisti Waniita mnashinalisti Na mimi ni binadamu tu, Kwani hilo halitoshi? Nchi zinajiwakia Mamama wakiomboleza, wakilia Tumbi ya watoto wakiumia na maneno yote tunayotumia             kuuana na kuangamia Ewe mto Tumesimama pambizoni mwako machozi yakitudondoka             yakichanganyika moyoni mwako.

Touch Me

Nitakapo kizuizini Nitamwomba yoyote mwendani             aniguse                         taratibu                         polepole                                     lakini                                     kwa yakini! Niguse tena Unijuze tena Unifunze tena                         maisha yalivyo                         maisha yaonjavyo                                                 ladha yake ilivyo Nipo hapa nimekukabili Niguse tena tafadhali! Niguse! Niguse!

The Word Cutter

Zacheka nami zangu chekeo                zacheka zafurahika Sina mawazo    kichwani leo                Bado hayajarauka … Nadhani ni asubuhi                imeanza kuchipuka Nayo ndiyo sababu                ya moyo kuliwazika na huu mdundo mtamu                mwema ulotandazika Najichekea … kwani najua vyema kwamba sijazoea hali hii tabasama ijitembezayo kwa shairi na kwa ngoma ikichezacheza nami … […]

The Voice?

Shingo zetu zimechongoka             asubuhi kuilekea lakini usiku wasogea             ukichimba misingi ya nyumba,                       na ukuta wa dakika nyumba                       kuizunguka. Kifo kimeadhimishwa na ule wakati uliotandazika                       mpaka kila cha zamani kimesahaulika isipokuwa majani makavu yalokauka Mitini, mara kwa mara, yakitingisika    Ati n’nani aliyesikia sauti?    Kama kwamba kuna mtu huko mbinguni […]

In Prison (Kifungoni)

Kwa kuangulia juu mbinguni na kulia sana kwa matumaini samawati imeingia                               mwangu machoni. Kwa kuota mahindi mashambani na kulia sana kwa mahuzuni manjano imeingia                               mwangu machoni. Waache majemadari waende vitani Wapenzi waende bustanini Na waalimu mwao darasani,             Ama mimi, tasubihi nipeni             Na kiti cha kale, za zamani             Niwe vivi nilivyo […]